1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mapendekezo Kosovo iwe huru.

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2u

Marekani pamoja na nchi za Umoja wa Ulaya zimewasilisha mswada wa azimio la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha jimbo la Kosovo kupewa uhuru wake kwa usimamizi wa jumuiya ya kimataifa.

Mswada huo umewasilishwa ingawa Russia iliupinga vikali.

Azimio hilo linaunga mkono mpango wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Martti Ahtisaari, unaopendekeza jimbo hilo la Serbia, ambalo limekuwa likisimamiwa na Umoja wa Mataifa, lipewe uhuru lakini lisimamiwe na Umoja wa Ulaya.