1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Marekani yapiga kura ya veto kuihami Israel.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtd

Marekani imepiga kura ya veto dhidi ya muswada wa azimio uliodhaminiwa na mataifa ya Kiarabu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa ambao ungeishutumu Israel kwa shambulio lililosababisha maafa makubwa katika eneo la kaskazini la ukanda wa Gaza mapema wiki hii.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton amesema kuwa ametumia kura ya veto, kwasababu muswada huo haukuwa na uwiano na umeelemea upande mmoja.

Israel imesema kuwa shambulio hilo la makombora ambalo limeuwa raia 18 wa Palestina , wengi wao wakiwa wanawake na watoto, katika mji wa Beit Hanun Jumatano iliyopita lilikuwa la bahati mbaya.