1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Mataifa makubwa yaahirisha kura kuiwekea vikwazo Iran.

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLp

Mataifa makubwa yenye nguvu yamekubaliana kuchelewesha kura juu ya vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran. Katika mkutano mjini New York , wanachama watano wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani na umoja wa Ulaya wamekubaliana kusubiri hadi Novemba , wakingojea ripoti ya kiongozi wa shirika la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic Mohammed El Baradei pamoja na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana.

Ilikuwa ni wazi kabla ya mazungumzo kuwa Russia na China zilitaka kutoa kwa shirika hilo la umoja wa mataifa IAEA muda zaidi wa kufanya uchunguzi.

Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zilitaka kuendelea na awamu ya tatu ya vikwazo dhidi ya Iran kwa kukataa kusitisha shughuli zake za urutubishaji wa madini ya Urani, ambapo mataifa ya magharibi yanashaka kuwa hali hiyo inaweza kutumiwa kuunda silaha za kinuklia. Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.