1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Mbinyo kuhusu kujiuzulu kwa Wolfowitz waongezeka.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6e

Kundi la wafanyakazi wa benki kuu ya dunia limeeleza wasi wasi wake kuwa mzozo unaomkabili rais wao Paul Wolfowitz unaharibu hadhi ya taasisi hiyo.

Katika barua , kundi hilo la maafisa 32 limeonya kuwa kashfa hiyo inaharibu hadhi ya benki hiyo.

Barua hiyo pia imetoa wito wa kuchukuliwa hatua kamili na za wazi.

Wolfowitz anakabiliwa na miito ya kujiuzulu baada ya kujitokeza taarifa kuwa ameamuru ongezeko kubwa la mshahara na kumpandisha cheo hawara wake, ambaye alikuwa mfanyakazi wa benki hiyo.

Wakati huo huo , Wolfowitz amepata wakili mwenye hadhi ya juu na ameiandikia bodi ya utendaji kuhusiana na hali yake ya baadaye, akiishutumu kwa kutomtendea haki.