1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Miripuko ya Algiers yalaaniwa

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAJ

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali uripuaji wa mabomu mjini Algiers nchini Algeria hapo Jumaatano ambapo watu 33 wameuwawa na wengine zaidi ya 220 kujeruhiwa.

Baraza hilo limesema yoyote yule aliepanga,kugharamia na kutekeleza mashambulizi hayo lazima afikishwe mbele ya sheria.

Hatua za usalama zimeimarishwa nchini kote Algeria hususan katika vituo vya polisi.Vizuizi vya barabarani pia vimewekwa kwenye miji yenye harakati kubwa za usafiri wa magari.Wapelelezi wanalenga msako wao kwa tawi la mtandao wa kundi la kigaidi la Al Qaeda linalojulikana kama al Qaeda katika eneo la Maghreb ambalo limedai kuhusika na uripuaji huo wa mabomu.

Serikali ya Algeria inahofu kuzuka mashambulizi zaidi ya Waislamu wa itikadi kali.