1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mkutano wa Libya kujadili mgogoro wa Darfur

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlS

Wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watakutana baadae mwezi huu kutafuta njia ya kurejesha amani katika jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan.Mkutano huo unatazamiwa kufanywa tarehe 15 na 16 mwezi huu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.Majadiliano ya kisiasa kuhusu Darfur yalikuwa yakiongozwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Jan Eliasson na Salim Ahmed Salim wa Umoja wa Afrika.Lengo la mkutano wa Tripoli ni kutazama maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miezi miwili iliyopita,kutathmini njia ya kutekeleza mpango wa suluhisho mgogoro wa Darfur pamoja na kuchunguza mapendekezo ya hatua zinazofaa kuchukuliwa.Kwa mujibu wa wataalamu wa kimataifa,watu wapatao 200,000 wamepoteza maisha yao katika mgogoro huo wa miaka minne.