1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mswada kuhusu Israel kupigiwa kura na Baraza la Usalama

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtr

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo litapiga kura kuhusika na mswada wa kulaani shambulio la Israel katika Ukanda wa Gaza pamoja na mashambulio ya makombora yanayoafanywa na Wapalestina dhidi ya Israel.Mswada huo uliopendekezwa na Qatar kwa niaba ya wanachama wa Kiarabu,umepunguzwa makali ili kuyaridhia madola ya magharibi.Hata hivyo,inadhaniwa kuwa Marekani iliyo mshirika mkuu wa Israel,itatumia kura ya turufu kuupinga mswada huo unaotoa mwito kwa Israel moja kwa moja isitishe operesheni zake za kijeshi zinazowatia hatarini raia wa Kipalestina katika maeneo yaliokaliwa,ikiwa ni pamoja na Jerusalem ya Mashariki.Vile vile mswada huo unatoa mwito kwa Israel kuondosha vikosi vyake vilivyo ndani ya Ukanda wa Gaza na virejee vilikokuwepo kabla ya tarehe 28 Juni mwaka huu.