1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mwito wa kuwalinda wanawake na wasichana Darfur

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkv

Viongozi mashuhuri wa kike wametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kujitahidi zaidi kuwalinda wanawake dhidi ya ubakaji katika jimbo la magharibi la Darfur nchini Sudan.Katika barua wazi iliyochapishwa na magazeti mbali mbali duniani,viongozi mashuhuri wa kike kama waziri wa nje wa zamani wa Marekani Madeleine Albright,rais wa zamani wa Ireland Mary Robinson na aliekuwa waziri mkuu wa Ufaransa Edith Cresson wanatoa mwito wa kupeleka Darfur vikosi vya amani vyenye uwezo wa kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya ubakaji.Viongozi hao na wanaharakati wanasema, wanawake na watoto wadogo wa kike wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa.Wakaeleza kuwa,kila siku ubakaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake na wasichana,hutumiwa kama silaha,katika vita vya Darfur.Maandamano makubwa yamepangwa kufanywa siku ya Jumapili,katika nchi mbali mbali kuukumbusha ulimwengu mgogoro wa Darfur.