1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Nchi ziimarishe taratibu dhidi ya silaha za kibailojia

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqw

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan amezitaka nchi 155 ziimarishe taratibu za kimataifa dhidi ya silaha za kibailojia.

Akifungua mkutano wa kutathmini mkataba juu ya silaha hizo mjini New York leo hii, katibu mkuu amesema kuwa hatari zimeongezeka tokea miaka mitano iliyopita baada ya mkutano uliomalzika kwa mfarakano.

Mkataba huo ni juu ya kuzuia kuunda na kulundika silaha za kibaolojia.

Juhudi za kuweka taratibu za kuhakikisha utekelezaji wa mkataba huo zimekataliwa na nchi kadhaa ikiwemo Marekani.