1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Pendekezo kuidhinisha vikosi vya Darfur

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnk

Uingereza na Ghana zinatazamia kupendekeza azimio la kuidhinisha vikosi vya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa,kusaidia kumaliza mgogoro wa miaka minne katika jimbo la Darfur,nchini Sudan. Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Emyr Jones Parry amesema,ni matumaini yake kuwa azimio hilo litapitishwa na Baraza la Usalama,juma moja baada ya kupendekezwa.Mpango huo unapendekeza kupeleka Darfur,wanajeshi 23,000 wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.Lengo ni kuwasaidia wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika ambao tayari wapo Darfur.Mapema mwezi huu,serikali ya Sudan ilikubali kuruhusu vikosi vya kimataifa katika jimbo la mgogoro la Darfur.