1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Rais wa Sudan atuma baruwa Umoja wa Mataifa

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMy

Rais wa Sudan anatuma baruwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuelezea kujifunga kwake kwa uwekaji wa maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusaidia kukomesha umwagaji damu huko Dafur.

Uwekaji wa kikosi hicho utakuwa utekelezaji wa hatua ya pili ya mpango wa Umoja wa Mataifa ambao utakamlishwa na awamu ya tatu ya uwekaji wa kikosi cha wanajeshi 22,000 mchanganyiko wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika jimbo hilo lilioko magharibi mwa Sudan.

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amekuwa akitowa maelezo ya kutatanisha juu ya kujifunga kwake na mpango huo na mapema mwaka huu Ban amemtaka kuelezea kukubali kwake awamu hiyo ya pili ya mpango huo kwa maandishi.

Kwa mujibu wa balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa Abdalmahmood Abdalhalim baruwa ya Bashir inaelezea kujifunga kwake na mpango huo lakini pia inataka kujuwa juu ya masuala ya operesheni,taratibu na sheria.