1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Rwanda katika hatari ya mauaji ya kikabila

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ0
Mapigano ya Mogadishu
Mapigano ya MogadishuPicha: picture-alliance/ dpa

Rwanda kukabiliwa na duru mpya ya umwagaji damu wa kikabila iwapo itashindwa kuwachukulia hatua wale wanaowauwa mashahidi na wahanga walionusurika na maujai ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binaadamu la Human Right Watch lenye makao yake mjini New York Marekani madarzeni ya wahanga walionusurika wa mauaji ya kimbari na watu wengine waliohusika kwenye mchakato wa mahkama za kienyeji za gacaca zinazoendesha kesi za watuhumiwa wa mauaji hayo wameuwawa katika miaka ya hivi karibuni.

Repoti ya shirika hilo imesema hapo mwezi wa Novemba mauaji ya muhanga aliyenusurika wa mauaji ya kimbari ambaye mjomba wake ni hakimu wa mahkama za gacaca yalichochea mauaji ya kulipiza kisasi ya watoto wanne na watu wazima wanne.

Makundi ya wahanga walionusurika na mauaji ya kimbari yanakadiria kwamba hutokea vifo 20 vya wahanga hao kila mwaka katika miaka ya hivi karibuni.