1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Serikali ya Palestina yatakiwa kuwa na msimamo wa kuleta amani.

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGh

Maafisa wa kundi linaloshughulikia suala la amani ya mashariki ya kati wameitolea wito serikali mpya ya Palestina kuhakikisha kuwa inawajibika katika kuleta amani na kuitambua Israel. Kundi hilo, ambalo linajumuisha Marekani, umoja wa Ulaya, Russia na umoja wa mataifa , pia limesema kuwa vikwazo juu ya msaada wa moja kwa moja kwa mamlaka ya Palestina vitaendelea kwa hivi sasa.

Hapo kabla Marekani na umoja wa Ulaya zilionekana kulegeza msimamo wao kuelekea serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina baada ya pande zote mbili kusema kuwa watafanya mazungumzo na mawaziri ambao hawatoki katika chama cha Hamas. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kwenda katika eneo hilo mwishoni mwa mwezi huu kwa mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina.