1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Sudan yashutumiwa kwa kufanya mauaji Darfur.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0q

Shirika la umoja wa mataifa la haki za binadamu limeyashutumu majeshi ya usalama ya Sudan kwa kuhusika katika mauaji ya zaidi ya watu 100 kusini mwa jimbo la Darfur .

Kamishna wa haki za binadamu Louise Arbour ametaka kufanyike uchunguzi huru kuhusu madai kwamba watu wenye silaha kali walihusika katika mashambulizi dhidi ya vijiji katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu.

Ripoti ya umoja wa mataifa imesema kuwa ,ashahidi wamewatambua wengi wa watu hao waliofanya mashambulizi kuwa ni walinzi wa mpakani wanaozungumza Kiarabu.

Serikali ya Sudan imekuwa wakati wote wakikana kuwa walinzi wao wanahusika katika mauaji katika jimbo la darfur ambako watu zaidi ya 200,000 wameuwawa na zaidi ya milioni mbili kukimbia makaazi yao katika muda wa miaka minne iliyopita.