1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Sudan yatishiwa kuwekewa vikwazo vikali zaidi

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJA

Uingereza na Marekani zimeionya serikali ya Sudan kuwa hatua zitachukuliwa ikiwa itaendelea kukataa kutoa idhini ya kupelekwa vikosi vya kimataifa kulinda amani katika jimbo la mgogoro la Darfur magharibi mwa Sudan.Mjini New York,balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa,Emyr Jones Parry amesema,hatua za kuishinikiza zaidi Sudan zapaswa kuchukuliwa,ikiwa serikali ya Khartoum haitofanya maendeleo kuhusu suala hilo.Hata Marekani imetishia kuchukua hatua kali zaidi.Hadi hivi sasa,Rais wa Sudan Omar el-Bashir amekataa kuruhusu vikosi vya ziada vya Umoja wa Afrika na hata vikosi vya Umoja wa Mataifa,kuingia nchini humo kuwalinda raia wanaoshambuliwa na wanamgambo wenye asili ya Kiarabu.