1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa waidhinisha askari kwenda Darfur, Sudan

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByF

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha mpango wa kuwapeleka wanajeshi zaidi ya elfu ishirini na tatu na polisi wa kuwalinda raia katika eneo la Darfur linalokumbwa na vita.

Pendekezo hilo la kupeleka kikosi kinachojumuisha majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa tayari limewasilishwa kwa balozi wa Sudan wa Umoja wa Mataifa ili lipate idhini ya serikali ya Sudan.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeyataka makundi yote husika yaunge mkono mchakato huo wa kisiasa, yakome kuwashambulia raia pamoja na wanajeshi wa kuweka amani na pia yasaidie katika harakati za kutoa misaada ya kibinadamu.