1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa waidhinisha azimio kuhusu mauaji ya wayahudi.

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio dhidi ya wanaokanusha mauaji ya wayahudi wakati wa utawala wa manazi.

Azimio hilo liliwasilishwa na Marekani na kuungwa mkono na mataifa zaidi ya mia moja.

Azimio hilo linapinga jitihada zinazoendelezwa kukanusha mauaji wa wayahudi ambapo maafisa wa kibalozi walisema azimio hilo lilidhamiriwa Iran ambayo imekuwa mara kwa mara ikitoa kauli za kutilia shaka iwapo mauaji hayo yalitokea kweli.

Serikali ya Iran ilishutumiwa kimataifa pale ilipoandaa kongamano la siku mbili mwezi Disemba mwaka uliopita kuchunguza iwapo wayahudi milioni sita waliuawa na manazi wakati wa vita vya pili vya dunia.