1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Umoja wa Mataifa waoanya kuhusu janga la kiutu nchini Irak

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwL

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi-UNHCR-limeonya kuwa janga la kiutu nchini Irak linalosababishwa na mgogoro nchini humo,linazidi kuwa kubwa kwa sababu ya uhaba wa misaada ya kimataifa.Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR,shirika hilo limeshtushwa jinsi jumuiya ya kimataifa inavyojikokota kukabiliana na tatizo la watu waliopoteza makazi yao.Hadi Wairaki milioni 1.6 wamelazimika kuondoka makwao.Wakati huo huo kila mwezi,takriban wakimbizi 100,000 wanawasili Syria na Jordan na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa serikali za nchi hizo.