1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Umoja wa mataifa waukaribisha uamuzi wa Rwanda kuondoa hukumu ya kifo.

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBed

Kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa ameukaribisha uamuzi wa Rwanda wa kufuta adhabu ya kifo. Louise Arbour ameisifu nchi hiyo kwa kuonyesha uongozi kwa vitendo, kutokana na kutangaza hatua hiyo siku ya Alhamis.

Uamuzi huo una maana pia kuwa zile nchi ambazo zimekataa kuwakabidhi watuhumiwa wa mauaji ya halaiki kwa mahakama nchini Rwanda kwasababu wanaweza kuhukumiwa kifo wanaweza sasa kufanya hivyo.

Umoja wa Ulaya pia umekaribisha hatua hiyo ukisema kuwa ni hatua muhimu kuelekea maridhiano katika nchi hiyo miaka 13 baada ya kutokea mauaji ya kimbari na watu zaidi ya 800,000 Watutsi na Wahutu kuuwawa.