1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. UN kutuma ujumbe Kosovo.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCO

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kutuma ujumbe katika jimbo la Kosovo baadaye mwezi huu ili kuweza kutathmini hali katika jimbo hilo la Serbia .

Balozi wa Uingereza katika umoja wa mataifa Emyr Jones Parry amewaambia waandishi wa habari kuwa ujumbe huo huenda ukajumuisha mabalozi kutoka nchi zote 15 wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Baraza hilo linaangalia pendekezo lililotolewa na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Martti Ahtisaari kuhusu hali ya baadaye ya jimbo hilo lenye wakaazi wengi wa asili ya Kialbania.

Akizungumzia pendekezo la Ahtisaari rais wa Serbia Vojislav Kostunica ametaka kutumwa kwa ujumbe mpya wa wawakilishi wa umoja huo katika jimbo hilo.

Mpango huo utaipatia Kosovo uhuru chini ya uangalizi wa jumuiya ya kimataifa.

Serbia inapinga pendekezo hilo, na Russia imeonyesha kuwa huenda ikawa tayari kutumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzuwia mpango huo.