1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Upinzani mpya unachelewesha kura kupigwa

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2s

Urussi na China zimezusha upinzani mpya utakaoweza kuchelewesha kura kupigwa kuhusu azimio linalotazamia kuweka vikwazo dhidi ya Korea ya Kaskazini kwa sababu ya jaribio lake la kinuklia.Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,John Bolton amesema,kimsingi mabadilisho yaliyopendekezwa na Moscow na Beijing yanahusika na mbinu-ufundi na hivyo bado upo uwezekano wa kura kupigwa leo hii.Lakini balozi wa China katika Umoja wa Mataifa,Wang Guangya amesema,bado hakuna makubaliano yaliopatikana.Wanachama 5 wa kudumu katika Baraza la Usalama pamoja na Japan zilipanga kukutana mapema leo hii kabla ya wanachama wote 15 wa baraza hilo kuyajadili mageuzi yaliyofanywa.Mswada wa sasa unaitaka Korea ya Kaskazini itoe silaha zake zote za kinuklia,lakini unaeleza wazi wazi kuwa hatua ya kijeshi haitochukuliwa dhidi ya nchi hiyo.