1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Upunguzaji wa umasikini Afrika bado uko nyuma.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtx

Umoja wa mataifa unasema kuwa licha ya mafanikio machache, upunguzaji wa umasikini katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara bado uko nyuma ya malengo.

Umesema katika ripoti kuwa hakuna lengo la maendeleo ya Milenia ya umoja wa mataifa litakalofikiwa hadi kufikia muda uliopangwa wa 2015.

Yakiidhinishwa mwaka 2000 , malengo manane yalikuwa yanalenga katika kupima maendeleo kuelekea kupunguza umasikini.

Ripoti hiyo imesema kuwa zaidi ya asilimia 40 ya watu wanaoishi eneo la kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

Zaidi ya hayo , idadi ya watu wanaokufa kutokana na ukimwi imeendelea kuongezeka.

Taarifa hiyo ya awali imetolewa wakati viongozi wa mataifa manane yenye viwanda duniani wanakutana nchini Ujerumani.

Umoja wa mataifa umesema kuwa mataifa fadhili yanahitaji kwenda haraka zaidi iwapo yanataka kutimiza ahadi zao za kuongeza kwa mara dufu misaada kwa Afrika ifikapo mwaka 2010.

Taasisi hiyo imesema kuwa kitu kizuri kwa bara la Afrika ni ukuaji wa uchumi na pia kupungua kwa mizozo ya kijamii.