1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Uteketezaji wa misitu huathiri vibaya ujoto wa ardhi

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ5

Ripoti mpya ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa-FAO inasema,ulimwengu unaendelea kuteketeza misitu kwa kiwango kisichoweza kukubalika.Uteketezaji huo unaathiri vibaya sana ujoto wa ardhi.Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya FAO,eneo la misitu,maradufu ya eneo la jiji la Paris,hutoweka kila siku.Wagombea mazingira hasa wanahofia kile kiwango cha misitu inayoteketezwa katika nchi za Amerika ya Kati na barani Afrika. Umoja wa Mataifa unasema,wakati miradi ya kupanda miti imefanya maendeleo ya wastani katika nchi za Ulaya na Amerika ya Kaskazini,katika nchi zinazoendelea,matatizo ya kiuchumi hugubika masuala yanayohusika na mazingira.