1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vijana washtakiwa njama ya kushambulia wanajeshi

9 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3u

Nchini Marekani watu 6 wamekamatwa katika jimbo la New Jersey na kushtakiwa kupanga njama ya kutaka kushambulia kituo cha kijeshi cha Fort Dix.Washtakiwa hao ni wanaume vijana wa Kiislamu,waliotokea Yugoslavia ya zamani na Mashariki ya Kati.Miongoni mwao ni mfanyakazi anaewasilisha chakula cha pizza.Inadhaniwa kuwa mfanyakazi huyo aliitumia kazi hiyo kukichunguza kituo cha kijeshi.Maafisa wa Kimarekani wamesema, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaowahusisha washtakiwa hao na makundi ya kigaidi ya kimataifa kama vile Al-Qaeda.