1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Viongozi kuwajibika zaidi kupiga vita Ukimwi

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnX

Siku ya Ukimwi duniani iliadhimishwa hiyo jana sehemu mbali mbali za ulimwengu.Mashirika ya afya yamesema,ugonjwa huo ni kitisho kikubwa kwa binadamu,ambacho hakijawahi kushuhudiwa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amesisitiza jinsi ugonjwa huo ulivyoripuka na ametoa mwito kwa wanasiasa kuwajibika zaidi.Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika,ni eneo lililoathirika zaidi lakini maafisa wa siha wanaonya kuwa sasa Ukimwi unatapakaa kwa haraka Asia ya Kusini vile vile.