1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru Burma

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I9

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari ameionya serikali ya kijeshi ya Burma juu ya athari za ukandamizaji wa upinzani nchini humo. Gambari alikuwa akiripoti juu ya ziara yake ya siku nne nchini Burma mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ametoa mwito kwa viongozi wa kijeshi kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.Wakati huo huo,amekaribisha taarifa iliyosema kuwa viongozi wa kijeshi wapo tayari kukutana na kiongozi wa upinzani Aung San Sun Kyi.

Hapo awali, serikali iliarifu kuwa Jemadari Than Shwe yupo tayari kukutana na kiongozi huyo wa upinzani, lakini kwa sharti kuwa ataacha kuwahimiza wafuasi wake kuipinga serikali ya kijeshi.