1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wajumbe wa Baraza la Usalama hawatokwenda kwenye mkutano wa Darfur

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,limefuta mpango wa kutuma ujumbe wake mjini Addis Ababa siku ya Jumatatu,kushiriki katika mazungumzo pamoja na serikali ya Sudan na Umoja wa Afrika, juu ya mgogoro wa Darfur.Balozi wa Peru katika Umoja wa Mataifa,Jorge Voto-Bernales ambae hivi sasa pia ni rais wa Baraza la Usalama amesema, wameshindwa kuafikiana juu ya mamlaka ya tume hiyo na ujumbe wa kuwasilishwa.Tarehe 31 Agosti,Baraza la Usalama lilipitisha uamuzi wa kupeleka Darfur kikosi cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 20,000 kulinda amani katika eneo hilo la mgogoro,magharibi mwa Sudan.Wanajeshi hao walitazamiwa kukipokea kikosi cha Umoja wa Afrika chenye matatizo ya kifedha na uandaaji.Majeshi hayo yameshindwa kukomesha mmuagiko wa damu.Rais wa Sudan,Omar al-Beshir lakini anakataa kabisa kuviruhusu vikosi vya Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur.