1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Wakubaliana juu ya kikosi cha Dafur

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByg

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hapo jana wamekubaliana juu ya kikosi cha pamoja kusaidia kuwalinda raia na kurudisha usalama katika jimbo lenye mgogoro la Dafur nchini Sudan kikosi ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa wa nyendo na kuzuwiya umwagaji damu.

Repoti ya kurasa 39 yenye kupendekeza mamlaka na muundo wa kikosi hicho mchanganyiko cha wanajeshi 23,000 na polisi itapalekwa kwa serikali ya Sudan kwa ajili ya kuidhinishwa.

Balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa Zalmay Kalilzad ambaye ni rais wa sasa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema sasa mpira uko kwenye uwanja wa Sudan.

Wataalamu wa Baraza la Usalama walikutana hapo jana mchana kujadili repoti hiyo na rasimu ya taarifa iliopendekezwa na Marekani ambayo inayaita makubaliano hayo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuwa ni maendeleo muhimu katika kuendeleza mchakato wa amani wa Dafur.