1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wito kupeleka Somalia vikosi vya kimataifa

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnU

Waziri Mkuu wa Somalia,Ali Mohamed Gedi ametoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuisaidia nchi yake iliyo katika njia panda hivi sasa.Akilihotubia Baraza la Usalama la Umoja wa Maataifa,Gedi alisema,vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vipelekwe Somalia kuchukua nafasi ya wanajeshi 1,500 wa Umoja wa Afrika waliopo nchini humo. Lakini,wanachama wengi katika Baraza la Usalama wamedhihirisha kuwa suala hilo haliwezi kuzingatiwa kwa hivi sasa.Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa,Emyr Jones Parry amesema,uwezekano wa kupeleka vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa,utaweza kuzingitiwa,kama utulivu fulani utapatikana Somalia na ikiwa makubaliano ya kisiasa yatapatikana katika majadiliano yaliyopangwa kufanywa katikati ya mwezi wa Julai kwa azma ya kuleta upatanisho wa kitaifa.