1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Wito kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCP1

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon amekaribisha juhudi ya hivi karibuni inayoshinikiza kupiga marufuku mabomu ya mtawanyo.Matamshi hayo yametolewa na msemaji wake baada ya nchi 46 kutoka jumla ya 49 zilizokutana Oslo nchini Norway kutoa ahadi ya kupata mkataba huo,ifikapo mwakani.Japan,Poland na Romania zimekataa kutia saini.Uingereza ambayo ni mtumiaji mkuu na huweka akiba kubwa ya mabomu ya mtawanyo na hata Ufaransa iliyo mtengenezaji mkuu wa mabomu hayo,ni miongoni mwa nchi zilizokubali kutia saini makubaliano hayo.Mataifa mengine muhimu kama Marekani,Israel,Urussi na China hayakuhudhuria kabisa mkutano huo mjini Oslo.