1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Baraza la usalama la UN lalaani mashambulio dhidi ya Bhutto

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DP

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga la wiki iliyopita dhidi ya msafara wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto mjini Karachi.

Baraza la usalama limelitaja shambulio hilo kuwa kitendo kiovu cha kigaidi.Katika taarifa baraza hilo la usalama lenye wanachama 15 limezitolea mwito nchi zote kushirikiana katika kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na kitendo hicho.Halikadhalika baraza hilo limesisitiza kwamba litafanya kila liwezalo kupambana na ugaidi wa aina yoyote duniani.