1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Bush atangaza vikwazo zaidi kwa Myanmar

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMd

Rais George Bush wa Marekani katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alielezea vikwazo zaidi vya nchi yake dhidi ya utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Rais Bush pia alisema serikali yake inaunga mkono mapambano ya kutafuta demokrasia katika nchi za Iraq, Afghanistan na Lebanon.

Aidha amesema anakubaliana na hoja ya kuongezwa idadi ya wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la umoja huo, lakini akaitaja Japan tu kuwa ndiyo inayoweza kupata nafasi hiyo.

Utawala wa kijeshi wa Junta kwa sasa uko katika mbinyo mkubwa wa watawa wa madehebu ya kibuddha wanaongoza maandamano ya amani kwa siku ya saba sasa, wakichagiza demokrasia nchini humo.

Nchini Myanmar kwenyewe, serikali ya nchi hiyo imetangaza amri ya kutotembea usiku katika miji ya Rangoon na Mandalay ikiwa ni katika hatua za kupambana na mandamano hayo.

Utawala huo pia umeiweka miji hiyo miwili chini udhibiti wa vikosi vya jeshi kwa muda siku 60.