1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Katibu Mkuu mpya kujulikana leo ?

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4j

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linatarajiwa kutoa uamuzi juu ya mtu atakaechukua wadhifa wa ukatibu mkuu wa Umoja huo kumfuatia Kofi Annan anaemaliza muda wake mnamo mwezi wa desemba.

Mgombea anaetarajiwa kupitishwa ni waziri wa mambo ya nje wa Korea ya Kusini bwana BAN KI MOON. Wagombea wengine wameshajitoa katika kinyang’anyiro hicho.