1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.Majeshi ya muunagno kubakia Irak kwa kipindi kipya cha miezi 12

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoU

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli moja uamuzi utakao yawezesha majeshi ya muungano yanayo ongozwa na Marekani kubakia nchini Irak kwa kipindi kipya cha miezi 12 ijayo.

Azimio hilo limefuatia ombi lililotolewa na serikali ya waziri mkuu wa Irak Nouri al Maliki ili kuweza kuidhibiti hali ya usalama nchini mwake wakati ambapo serikali yake inajitahidi kuunda vikosi vya usalama.

Kwa mujibu wa uamuzi huo wa baraza la usalama la umoja wa mataifa vikosi vya muungano vitabakia nchini Iraki hadi tarehe 31 Desemba mwaka 2007.

Marekani ina zaidi ya wanajeshi 150,000 nchini Irak huku kukiwa na wanajeshi wengine kutoka nchi 40 washirika wake wanaohudumu nchini humo.

Waziri mkuu wa Irak Nouri al Maliki ametoa ombi hilo wakati mauaji ya kimadhehebu yakizidi nchini Irak.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan ameonya kuwa nchi hiyo inakaribia kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.