1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Pande nne zinazoshughulikia amani ya mashariki ya kati zalaumiwa

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fd

Mjumbe wa umoja wa mataifa na mataalamu wa haki za binadamu John Dugard amesema kwamba ataihimiza taasisi hiyo ya kimataifa ijiondoe kwenye uanachama wa pande nne zinaoshughulikia maswala ya mashariki ya kati iwapo pande hizo hazitazingatia juu ya haki za kibinadamu za Wapalestina.

Bwana Dugard ambae anasimamia maswala ya haki katika maeneo ya Palestina amesema kuwa pande hizo nne zikiwemo Urusi, Umoja wa Ulaya, Marekani na Umoja wa Mataifa zimeshindwa katika majukumu ya kuwalinda Wapalestina.

Profesa huyo mstaafu kutoka Afrika Kusini amefahamisha kuwa pande zinazoshughulikia amani ya mashariki ya kati zinashindwa kutekeleza jukumu lake vilivyo kutokana na ushawishi mkubwa wa Marekani.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa marekani Condoleeza Rice ameanza ziara ya siku nne Mashariki ya Kati ambayo inakusudia kuweka msingi wa mkutano wa amani unaodhaminiwa na marekani uliopangiwa kufanyika mwezi Novemba.

Bibi Rice amekutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na waziri wa ulinzi wa Ehudu Barak.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani pia amekutana na rais wa mamalaka ya Plaetina Mahmoud Abbas na waziri mkuu Salaam Fayad.

Rice pia anatarajiwa kuzitembelea Misri na Jordan.