1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Pronk kurejea Sudan ?

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyH

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan bwana Jan Pronk anatazamiwa kurejea nchini humo baada ya kufukuzwa hivi karibuni. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amefahamisha hayo na kueleza kuwa bwana Pronk ataendelea kuwa mjumbe hadi mwishoni mwa mwaka, ambapo muda wake unamalizika. Bwana Pronk alifukuzwa Sudan baada ya kuandika katika tovuti yake kwamba ari ya majeshi ya nchi hiyo ilikuwa ya chini kutokana na kushindwa mara kwa mara katika jimbo la Darfur.