1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Rais wa Iran azikomoa nchi za magharibi juu ya mpango wake wa Nuklia

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMQ

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amerudia tena msimamo wake kwamba nchi yake ina haki ya kuwa na technologia ya kinuklia kwa ajili ya matumizi ya amani.

Akihutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini Newyork nchini Marekani rais huyo aliipinga miito mingine ya kuitaka nchi yake ikomeshe shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium akisema Tehran katu haitozisujudia nchi zinazofanya maamuzi yake kwa njia ya kiburi na jeuri kwa kujiona zenye nguvu.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy akizungumzia juu ya Iran alisema itakuwa hatari kubwa mno ikiwa Iran itaachiwa itengeneze Bomu la Atomiki.Kansela Angela Merkel amesema nchi yake itaunga mkono vikwazo vikali dhidi ya Iran ikiwa haitokubali kusimamisha mpango wake wa Kinuklia.Aidha ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kutogawika katika kuishughulikia Iran. Kutokana na mivutano ya muda mrefu kati ya Iran na jumuiya ya kimataifa juu ya shughuli zake Rais Mahmoud Ahmedinejad alitangaza katika hotuba yake hapo jana kwamba mzozo huo wa kinuklia kati ya taifa lake na jumuiya hiyo umekwisha na kwamba sasa jukumu lipo kwenye mikono ya shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Kinuklia IAEA.