1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Ufaransa na Rwanda katika juhudi za kurejesha uhusiano

25 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMs

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na Ufaransa wamekuwa na mazungumzo kwa mara ya kwanza toka kuvunjika kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili mwaka jana.

Waziri wa Nje wa Ufaransa Bernad Kouchner alikutana na mwenziye wa Rwanda Charles Murigande pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rwanda ilivunja uhusiano na Ufaransa baada ya jaji mmoja wa nchi hiyo kumtia hatiani Rais Paul Kagame kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Mauaji hayo yalianza baada ya kudunguliwa ndege aliyokuwemo Rais Habyarimana.

Rwanda imekuwa ikituhumu Ufaransa kwa kuwaunga mkono wahutu waliyoshiriki katika mauaji hayo na kushindwa kwake kutoa ushirikiano kwenye uchunguzi wa chanzo chake.