1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Umoja wa Mataifa waiondolea vikwazo wa almasi Liberia

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6J

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana limeondoa vikwazo kwa Liberia kusafirisha almasi, likisema kuwa nchi hiyo imepiga hatua katika kudhibiti matumizi haramu ya fedha za almasi.

Wanachama 15 wa baraza hilo kwa kauli moja walikubaliana kuliondoa azimio hilo na vikwazo lililoundwa na Marekani mwaka 2003.

Hii ni mara ya pili kwa baraza hilo kupiga kura inayoonesha kuridhishwa kwake na uongozi wa rais mpya wa Liberia Hellen Johnson Sirleaf.

Rais huyo wa Liberia ni rais wa kwanza mwanamke barani afrika na alichaguliwa mwaka jana baada ya kumalizika kwa miaka 14 ya vita vya kikabila nchini humo.

Mwezi Juni mwaka jana Baraza hilo lilipiga kura kuondoa azimio la vikwazo dhidi ya bidhaa za mbao za Liberia.

Almasi na bidhaa nyingine kama vile mbao zinatuhumiwa kusafirishwa na kuuzwa nje ambapo fedha zilizopatikana zilitumika kununua silaha, zilizochangia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia, Siera Leone na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.