1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neymar atambulishwa rasmi Ufaransa

Sekione Kitojo
7 Agosti 2017

Ligi ya ufaransa yaanza kutimua vumbi, Paris St. Germain yashinda bila mchezaji wao nyota aliyesajiliwahivi karibuni kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia Mbrazil, Neymar

https://p.dw.com/p/2hpzw
Paris Saint-Germain Vorstellung neuer Spieler Neymar
Neymar akitambulishwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-KhelaifiPicha: Reuters/C. Hartmann

Msimu  wa  ligi nchini  Ufaransa  League 1 umefunguliwa rasmi mwishoni  mwa  Juma  ambapo katika  siku  ya ufunguzi  rasmi  wa  ligi  hiyo  siku  ya  Ijumaa  Monaco mabingwa watetezi  walifanikiwa  kupata  ushindi  wa mabao 3-2  dhidi  ya  Toulouse na  Jumamosi  Paris St. Germain  iliikandika  Amiens  kwa  mabao  2-0  bila  ya nyota  wao  Neymar  waliyemnyakua  hivi  karibuni  kutoka FC Barcelona  ya  Uhispania  kwa  kitita  cha  juu  kabisa cha  euro  milioni  222.  Hata  hivyo  kufunguliwa  kwa  ligi hiyo hakukuwa  kwa  kishindo  kuliko  PSG  kumsajili  nyota huyo  kutoka  Brazil , Neymar. Kocha  wa  PSG Unai Emery alisema , PSG  ni timu  kubwa  bila  ya  Neymar, lakini Neymar  anaiongezea  umaarufu .

Frankreich Neymar-Schriftzug auf dem Eifel-Turm
Mnara wa Eifel ulipambwa kwa rangi za klabu hiyo ya mjini Paris , PSGPicha: Getty Images/AFP/O. Morin

"Bila Neymar , PSG ni  klabu  kubwa lakini  pamoja  na Neymar inakuwa  kidogo  bora  zaidi, kidogo kubwa  zaidi na  pia  kuna  njia  tunaweza kumjumuisha  mchezaji  kama yeye, na  pia  kwa  wengine  ambao  ni  wachezaji  wazuri, tunaweza  kupiga  hatua, tunaweza  kuwa  timu  kubwa  na pia  ni  kweli kwamba  kwa  msisimko wa  mashabiki, muktadha  ni  mzuri, ni hali  nzuri  kabisa."

Paris Saint-Germain Vorstellung neuer Spieler Neymar
Neymar akiwa katika mkutano na waandishi habari baada ya kujiunga na PSGPicha: Getty Images/AFP/L. Bonaventure

Mchezaji  huyo  ambaye  donge  la  kumsajili  la  euro milioni  222  kutoka  Barcelona limefikia  rekodi  ya  dunia ya  uhamisho , amezuiwa kucheza mchezo  wake  wa kwanza  katika  msimu  mpya  kwa  kuwa  usajili  wake umemalizika  kwa  kuchelewa. Hata  hivyo  alitambulishwa kwa  mashabiki  wa  timu  hiyo katika  uwanja  wa  parc des Princes mjini  Paris  kabla  ya  mchezo  huo  kuanza.

Nani kuchukua  nafasi ya Neymah Barcelona ????

Swali  na tetesi  na  minong'ono  iliyomo  katika  vyombo vya  habari  kwa  hivi  sasa  ni juu  ya , nani  anachukua nafasi  ya  Neymar  katika  Barcelona. Kuna  majina kadhaa  yanayotajwa  ambapo  mazungumzo  yanaendelea na  maafisa  wa  timu  za  wachezaji  hao, ambapo  jina linalotajwa  sana  ni  Ousnane Dembele  wa  Borussia Dortmund  kijana  wa  miaka  19 kutoka  Ufaransa kuweza kuchukua  nafasi  hiyo  adimu  katika  kikosi  cha Barcelona. Pia yupo Philip Courtinho  wa  Liverpool , Mbrazil  ambaye Barca wameweka  kitita cha  milioni 132 kumtwaa  mshambuliaji  huyo. Ni  kipi  kitakachotokea katika  siku  na  wiki  za  kuelekea  mwishoni  mwa kufungwa  kwa  dirisha  la  usajili  mwezi  huu  ni swali  na kusubiri  na  kuona.

Bundesliga | 26. Spieltag | FC Schalke 04 vs Borussia Dortmund
Ousmane Dembele wa Borussia DortmundPicha: Getty Images/Bongarts/L. Baron

Kocha  wa  Manchester  Jose Mourinho anaweza  kunyakua taji  moja  la  Ulaya  ambalo  bado  hajawahi  kulipata , wakati  kikosi  chake  kitakapokutana  na  Real Madrid katika  kombe  la  UEFA  Super  Cup  kesho  Jumanne katika  mchezo  wake  wa  kwanza  kupambana  na  vigogo hao  wa  Uhispania  tangu  kutengana  nao mwaka 2013.

Mourinho , ambaye  timu  yake  ilishinda  kombe  la  ligi  ya Ulaya  Europa  League  msimu  uliopita na  kuokoa  kile ambacho  huenda  ni msimu  wa  kwanza  uliokatisha tamaa  chini  ya  kocha  huyo  kutoka  Ureno, aliiongoza Real Madrid  kupata  ubingwa  wa  La  Liga  kwa  kutia kibindoni  pointi  100  ikiwa  ni  rekodi  na  kushinda  kombe la  mfalme  katika  kipindi  kati  ya  mwaka  2010  hadi 2013.

Großbritannien Fußball Jose Mourinho von Manchester United
Kocha wa Man United Jose MourinhoPicha: Imago/Sportimage/S. Bellis

Mafanikio  yake  hayo hata  hayo  hata  hivyo katika Santiago Bernabeu waligubikwa , na  kukosana  na wachezaji  muhimu katika  kikosi  hicho  kama  Sergio Ramos na  Iker Casillas pamoja  na  migongano na  marefa na  wapinzani  pamoja  na  kushindwa  kunyakua  kombe la  Champions League, wakati  Real  iliposhindwa  katika nusu  fainali  kila  mwaka.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo/dpae,afpe,rtre,ape

Mhariri: Mohammed Khelef