1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni vigumu kutabiri atakayeshinda Marekani

Jane Nyingi
3 Novemba 2016

Zikiwa zimesalia siku tano tu kukamilika kampeini za uchaguzi wa urais  nchini Marekani, kura ya maoni ambayo imetolewa leo (03.11.2016) inaonyesha mchuano mkali kati ya Hillary Clinton na Donald Trump,

https://p.dw.com/p/2S70A
US TV Debatte Trump vs Clinton
Picha: Reuters/L. Nicholson

Ungwaji mkono Clinton umepungua dhidi ya Trump. Hata hivyo wapo baadhi ya wapiga kura hawajaamua  ni nani watakayechagua kati  ya wawili hao kuingia ikulu ya White houseKura hiyo ya maoni iliyofanywa na gazeti la NewYork Times likishirikiana na kituo cha televisheni cha CBS inaonyesha kuwa Hillary Clinton  anaongoza  na asilimia tatu tu dhidi ya mpinzani wake Donald Trump na hivyo kupunguza mwanya uliokuwepo kwa wiki kadhaa wa pointi tisa.Hiyo inamaana ni asilimia 45  ya wamarekani wanamuunga mkono Hillary huku asilimia 42 ikiwa upande wa mrepublican Trump. Hata hivyo wapiga kura wachache wamesema huenda wakabadilisha mawazo yao dakika za mwisho,huku asilimia 92 ikisema tayari ishaamua mgombea wao.Licha ya matokeo hayo ya kura ya maoni

US-Wahlkampf Schild
Mojawapo ya jimbo liloshiriki kura ya mapemaPicha: Getty Images/J. Sullivan

Hillary Clinton aliendelea na kampeini ya kutafuta kura katika jimbo la Arizona,ambalo ni  miongoni mwa majimbo Marekani ambayo kawaida yanadhibitiwa na chama cha Republican chake Donald Trump."Hebu fikiri ni Januari 20, 2017, na ni  Donald Trump wamesimama mbele ya Makao Makuu. Hebu fikiri  kuwa na rais anayedhalilisha akinamama, walemavu,ana watusi walatino,Wamerekani weusi, waislamu, na ni mtu wa kuwagoganisha watu badala ya kuwaleta pamoja. Ni mtu anaye mtusi yeyote anayepinga,anawasifu maadui  watu kama vladmir Putin, anayetaka vita na washirika wetu na hata kumtusi papa Francis.Iwapo Donald Trump atashinda huu,tutakuwa na kiongozi ambae hana mwelekeo na ambazo  mawazo yake ni hatari.” amesema Clinton

USA Poster / Transparente zu Präsidentschaftswahlen
Wafuasi wa Hillary Clinton jimbo la ArizonaPicha: Imago/Agencia EFE

Mwezi uliopita  kura za maoni za kitaifa zilimwonyesha Hillary akipata ungwaji mkono zaidi huku umaarufu wa Trump ukipungua  kutokana na madai ya kuwadhalilisha wanawake kingono. Hata hivyo sita kati ya wapiga kura 10 walisema madai hayo dhdi ya Trump yatachangia kwa kiasi kidogo sana kufanya uamuzi wao. Vilevile wapiga kura hawakuona chochote kipya na kashfa ya Clinton kutumia barua pepe binafsi kwa shughuli za kikazi alipokuwa waziri wa mambo ya nje  huku asilimia 62 ikisema ilikuwa akifahamu na tangazo hilo halitawabadili fikra. Hii leo Trump alikuwa  jimbo la Florida kusaka kura ambapo alimpiga vijembe mpinzani wake Clinton kuhusiana na sera yake ya uhamiaji ."Hillary anaunga mkono  miji inayohifadhi wahamiaji haramu kama  San Francisco, ambako Kate  Steinle  aliuawa na muhamiaji haramu na ambae amerejeshwa nchini mwake kwa lazima karibu mara tano.Utawala wa Trump utafuta ufadhili wa serikali kuu kwa miji yote yenye utaratibu wa kuwahifadhi wahamiaji haramu."

USA Vorwahlen Donald Trump in Mississippi
Mgombea wa urais Marekani Donald TrumpPicha: picture-alliance/ZUMA Press

Katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita  masoko ya fedha duniani yamkumbwa na ukosuko kutokana na matokeo ya  kura hizo za maoni zinazoonyesha wagombea hao wawili,Hillary na Trump wanakaribiana  katika ungwaji mkono.Thamani ya dola hata imeshuka dhidi ya Euro.

Mwandishi:Jane Nyingi/RTRE/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga