1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni wiki tu iliosalia kwa kombe la Dunia

20 Juni 2011

Timu mbalimbali za wanawake tayari zimewasili Ujerumani na zipo katika harakati za mwisho za matayarisho ya kuwania kulinyakuwa taji la mwaka huu, huku Ujerumani ikiwa ni mtetezi wa taji hilo kwa mara ya pili.

https://p.dw.com/p/11fgL
Ngoma inakaribiaPicha: DW

Homa ya kombe la dunia imetanda hapa Ujerumani. Tulikuwa tukihesabu miezi, wiki na sasa ni siku kadhaa tu kabla ya kuanza kombe la dunia la wanawake mwaka 2011.

Soccer Festival
Utaalamu uwanjaniPicha: Dannenberg

Mshikiliaji mara tano tuzo la mchezaji bora wa mwaka, anayetoka Brazil, Marta na mfungaji bora katika mashindano hayo, anayetoka Ujerumani, Birgit Prinz ni miongoni mwa majina makuu ya wachezaji watakao kuwepo katika mashindano hayo yanayoanza Jumamosi inayokuja, na yatakayoendelea kwa wiki tatu katika miji tisa ya hapa Ujerumani.

Timu 16 zinawania zawadi kuu huku tiketi zaidi ya laki 6 na elfu 70 za mashindano hayo zikiwa zimeshauzwa.

Miaka mitano baada ya kuandaliwa kombe la dunia la wanaume, matarajio ni makubwa kuwa nchi mwenyeji Ujerumani, kupitia wachezaji wake wakike watapata ushindi na kulinyakuwa taji la mashindano hayo kwa mara ya tatu mtawalia.

Mashindano hayo yanaanza Jumamosi tarehe 26 kwa mpambano kati ya timu mwenyeji, Ujerumani dhidi ya mabingwa wa taji la CONCACAF, Canada, katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin, unaopokea watazamaji 75,000. Na fainali inatarajiwa kugaragazwa mjini Frankfurt, tarehe 17 mwezi Ujao Julai.

Timu 16 zilizopo ni Ujerumani, Marekani, Australia,Korea kaskazini,Japan, Ufaransa,Norway,Uingereza, Sweden,New Zealand,Canada, Mexico, Equatorial Guinea kutoka Afrika pamoja na Nigeria , Brazil na Colombia.

Frauen Nationalmannschaft Birgit Prinz
Birgit Prinz wa timu ya taifa ya wanawake ya UjerumaniPicha: picture alliance/augenklick

Shauku kwa soka ya wanawake ni kubwa nchini Ujerumani kuliko katika nchi nyingine ile, na utangazaji wa mashindano haya mwaka huu unaonekana kuwa mkubwa kushinda mashindano ya siku za nyuma, na mwaka huu mpira huo utatangazwa kwa nchi zaidi ya 200 duniani.

Tiketi za mchezo wa ufunguzi zinakaribia kumalizika.

Soka ya wanawake ambayo katika siku za nyuma ilishutumiwa hususan katika mbinu ya unyakaji mpira,ambapo ulindaji lango ulisemekana kuwa duni, mchezo huo sasa umepiga hatua tangu kombe la kwanza la dunia mnamo mwaka 1991, na hili ni kutokana na mbinu kali walizonazo wachezaji kama Marta, Prinz na nyota wa zamani wa Marekani, Mia Hamm.

Frauen Fußball WM Japanische Nationalmannschaft
Kikosi cha Japan kinachoshiriki mashindano ya mwaka huuPicha: AP

Timu za Ujerumani na Marekani ndizo kwa kawaida zinazotamba katika mashindano haya, na zimefanikiwa kila mmoja kujishindia mara mbili taji hilo, huku Norway ikichukuwa ushindi mara moja mnamo mwaka 1995.

Hivyo basi kwa mara nyengine tena mwaka huu, timu hizo mbili ndizo kuu zinazotazamiwa, huku timu ya Colombia na Equatorial Guinea zikishiriki kwa mara ya kwanza.

Ujerumani inaanza katika kundi A dhidi ya Canada, na Nigeria, na Ufaransa.

Marekani inayoorodheshwa kuwa timu kuu imejizatiti katika kinyang'anyiro chao kwa kufuzu kwa ushindi wa kombe la Algarve nchini Ureno, na ipo katika kundi C na Korea kaskazini , Colombia na Sweden.

Japan, New Zealnad Mexico na Uingereza zipo kwenye kundi B, huku kundi D linazikutanaisha timu ya Brazil, Australia, Norway na Equatorial Guinea.

Mechi katika kiwango cha makundi zitaendelea hadi tarehe 6 mwezi ujao, huku timu mbili kuu zikifuzu kwa raundi ya mtoano zitakazoanza siku tatu baadaye.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Afpe/
Mhariri:Yusuf Saumu