1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niebel azuru Kenya

15 Agosti 2012

Waziri wa ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo wa Ujerumani, Dirk Niebel yuko katika ziara ya siku tano nchini Kenya kuanzia leo(15.08.2012).

https://p.dw.com/p/15pqY
Minister Dirk Niebel mit dem kenianischen Premierminister Raila Odinga in Naiobi (15.8.2011), Foto: Alfred Kiti, Korrespondent der Kisuaheli-Redaktion
Waziri wa ushirikiano wa maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel (kulia)Picha: DW

Ziara  hiyo  ina  lengo  la  kuadhimisha  miaka  50 ya  ushirikiano  wa  pamoja  kati   ya makanisa   mawili  yenye miradi yake  nchini  Kenya.  Pamoja  na  kukagua  miradi  kadha pia kutakuwa  na  mazungumzo  ya  kisiasa , hususan  na  waziri  mkuu Raila  Odinga.

Orodha  ya  mataifa  washirika  katika  ushirikiano  wa  maendeleo ni  ndefu, na  ina  idadi  karibu  ya  majina  60. Kenya  ni  moja  kati ya  washirika  muhimu  wa  ushirikiano  huo, ambapo  waziri Dirk Niebel  anaizungumzia  kama  " nguzo  ya  uthabiti",  katika  Afrika mashariki.

Tathmini  hii  ya  waziri  Niebel  kwa  ajili  ya  maendeleo ya  kiuchumi  na  ushirikiano , ina  misingi tofauti  ya  kimsingi. Na si kitu  cha  kushangaza  basi , kwamba  mwanasiasa  huyu  wa Ujerumani  katika  muda  wa  mwaka  mmoja,  hii  inakuwa  mara yake  ya   tatu  kwenda   Kenya.

Mwezi  August  mwaka  2011 Niebel  alikutana  na   rais  wa  Kenya Mwai  Kibaki  na  kutembelea  kambi  ya  wakimbizi  ya  Daabab , kambi  ambayo  inawahifadhi  watu  kutoka  katika  nchi  ya  Somalia inayokabiliwa  na  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe.

Mwanzoni mwa  maafa  ya  ukame  katika  eneo  la  Afrika  mashariki, ambapo hata   Kenya  iliathirika , kambi  hiyo  ambayo  ilikuwa  tayari  na wakimbizi  wanaofikia  nusu  milioni  ilivuka  kiwango  cha  uwezo wake  wa  kuwahifadhi  wakimbizi.

Ujerumani  inajihusisha  tayari kwa  miaka  mingi  pamoja  na  miradi  inayoendeshwa  na  umoja wa  mataifa  katika  kambi  hiyo  ya  Daadab. Kutokana  na  ukame na  matokeo  yake  waziri  wa  maendeleo  ya  Ujerumani  Niebel aliongeza  misaada  kwa  mataifa  ya  eneo  hilo  lote.

Pekee  Kenya ilipata  kiasi  cha euro  milioni  50  kwa  mujibu  wa   taarifa  rasmi  za serikali.

Mwanzoni  mwa  mwezi Februari mwaka  huu   waziri  Niebel alifanya ziara  katika eneo  la  Turkana  lililopo  katika  mpaka   na  Sudan  ya kusini  na  kueleza  kuwa  hali  katika  eneo  hilo  ni  ya  dharura. Miezi  sita  imepita  tangu  wakati  huo. Na  kwa  kuwa  mwanasiasa huyo  wa  Ujerumani  atatumia  siku  tano  katika  ziara  yake  nchini Kenya , ni  dhahiri  kuwa  suala  la  ukame  litakuwa  mada  muhimu ya  mazungumzo.

Muhumed Surow grieves following the burial of his 12-month-old daughter Liin Muhumed Surowlays at UNHCR's Ifo Extention camp outside Dadaab, Eastern Kenya, 100 km (60 miles) from the Somali border, Saturday Aug. 6, 2011. Liin died of malnutrition 25 days after reaching the camp, Mumumed said. The drought and famine in the horn of Africa has killed more than 29,000 children under the age of 5 in the last 90 days in southern Somalia alone, according to U.S. estimates. The U.N. says 640,000 Somali children are acutely malnourished, suggesting the death toll of small children will rise. (ddp images/AP Photo/Jerome Delay)
Ukame ambao unasababisha jangwa katika AfrikaPicha: AP

Mbali  na  msaada  wa  kibinadamu , Niebel  analenga  kuchukua hatua  endelevu  ya   kuisaidia  Kenya.

"Katika  ziara  hii  mbali  na  mazungumzo  ya  kisiasa  tutatembelea pia  miradi  inayoendeshwa  na  makanisa  ya  Kiinjili  na  Kikatoliki. Tunaweza  kufungua  mradi  wa  pande  tatu  pamoja  na  Israel katika  ziwa  Viktoria.

In this photo of Monday, Aug.8, 2011 and made available Wednesday, Aug.10, 2011, at the Kakuma Mission Hospital in Turkana region in northern Kenya a woman who identified herself as Chipure points at another woman. The two mothers exchanged blows as they held their wailing infants in their arms after one of the women tried to budge in the long line for children to receive treatment for severe malnutrition. The younger woman head-butted the other to the ground before hospital personnel intervened and separated them. Chipure, a mother of eight children, got a swollen lip from being head-butted. The incident at the Kakuma Mission Hospital illustrates the growing desperation in Kenya, as a famine in neighboring Somalia that has killed tens of thousands draws an international aid effort. (Foto:Tom Odula/AP/dapd)
Wakimbizi katika kambi ya Daadab nchini KenyaPicha: dapd

Waziri  mkuu  wa  Kenya  atakuwapo  na mwakilishi  wa   waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Israel. Hii inaonyesha , ni muhimu  kiasi  gani   ushirikiano  huu  kwa  serikali hizi  tatu. Na  ningependa  kutumia  fursa  hii, kuitembelea  taasisi  ya umoja  wa  mataifa  ya  mazingira  UNEP. Baada  ya  mkutano  wa mazingira  mjini  Rio  hiyo  ni mada  muhimu  sana".

Katika  mradi  kati  ya  Ujerumani , Israel  na  Kenya  ,mradi  huo unahusu   ufugaji  wa  samaki  ulioanzishwa  mwaka  1984. Mradi huo  unahusu  ufugaji  wa   aina  ya  samaki  wa  Sato, "Tilapia", ufugaji  wa  kuku, ng'ombe wa  maziwa, mbegu  za  mimea  ya matunda  na  miti.

Katika  maendeleo  ya  kisiasa  Kenya  itaendelea kupata  usaidizi  kutoka  Ujerumani. Mwishoni  mwa  mwaka  2010 nchi hiyo  baada  ya  majadiliano  na  serikali , ilipata  ahadi  ya kupatiwa  euro  milioni  130 kwa  muda  wa  miaka  mitatu. Mazungumzo  mengine  yatafanyika  katika  muda  wa  miaka  miwili ijayo  katikati  ya  mwaka  2013, baada  ya  uchaguzi  nchini  Kenya.

Mwandishi : Fürstenau, Marcel / ZR/ Sekione  Kitojo.

Mhariri: Othman  Miraji