1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiNiger

Niger kuipatia Mali mafuta ili kuboresha usambazaji wa umeme

17 Aprili 2024

Viongozi wa kijeshi wa Niger wanatazamiwa kumpatia jirani yake Mali, lita milioni 150 za mafuta ya dizeli zitakazotumiwa katika viwanda vya kufua umeme.

https://p.dw.com/p/4esX0
Nchi ya Mali yakabiliwa na tatizo la umeme
Nchi ya Mali yakabiliwa na tatizo la umemePicha: Patrick Batard/picture alliance/abaca

Hayo yameelezwa na ofisi ya rais wa Mali na kuongeza kuwa kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita, alikutana jana na waziri wa mafuta wa Niger, Mahaman Moustapha Barke na kukamilisha makubaliano hayo.

Takriban watu milioni 11 ikiwa ni karibu nusu ya watu wote nchini Mali wanatumia umeme. Lakini kampuni ya taifa ya nishati (EDM-SA) inakabiliwa na deni la dola milioni 330 na haina tena uwezo wa kuhakikisha usambazaji wa umeme katika mji mkuu wa Bamako na miji mingine ya Mali.

Mwezi Februari, Niger ilitangaza kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano kuhusu usambazaji wa dizeli kwa Burkina Faso, Mali na Chad, nchi zilizoorodheshwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani na zinazotawaliwa na tawala za kijeshi.