1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria-Boko Haram ni madhehebu gani ?

31 Julai 2009

Kiongozi wake Yusuf Mohammed auwawa.

https://p.dw.com/p/J0n2
Maiti- Maiduguri, Nigeria.Picha: AP

Taarifa kutoka Lagos, Nigeria, zinasema kwamba, Kiongozi wa madhehebu yenye itikadi kali ya kiislamu huko kaskazini mwa Nigeria,Mohammed Yusuf ameuwawa kwa kupigwa risasi katika gereza la polsi jana usiku.

Hii inafuatia siku kadhaa za machafuko katii ya wafuasi wake na vikosi vya ulinzi vya Nigeria yaliopelekea kuuwawa kwa watu kadhaa.Madhehebu ya BOKO HARAM alioyaongoza Mohammed Yusuf ni madhehebu gani na yanapigania nini ?

Mohammed Yusuf ,Kiongozi wa (Boko Haram),madhehebu inayopigania kutumiwa kwa wingi sharia ya kiislamu sehemu kubwa ya Nigeria,alitiwa nguvuni baada ya msako mkali ulioingiza ndege za helikopta za kijeshi,wanajeshi na polisi wenye silaha.Ghasia za wafuasi wake zilianza jumapili iliopita katika mkoa wa Bauchi.Hii ilifuatia kutiwa nguvuni na polisi baadhi ya wafuasi wa madhehebu wakitiiliwa shaka kuandaa njama kushambulia kituo cha poliisi.

BOKO HARAM ni madhehebu gani na inapigania nini ? Baadhi ya wakati ikiitwa "Watalibani wa Nigeria",wanachama wa madhehebu haya ni wafuasi wa mwanazouni wa kiislamu Mohammed Yusuf aliepinga mno elimu ya kimagharibi na alietaka sharia ya kiislamu itumike sehemu kubwa ya dola lenye wakaazi wengi kabisa barani Afrika la Nigeria.

Ikiwa na kambi yake Maiduguri,mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-mashariki wa BORNO,wafuasi wake ni pamoja na wahubiri wa zamani wa chuo kikuu na wanafunzi katika mikoa ya kaskazinii mwa Nigeria pamoja nayo Kano,Yobe,Sokoto na Bauchi.Pia hata watu wasiojua kusoma wala kuandika na vijana wasio na kazi.

"BOKO HARAM"-maana yake ni "elimu ya kimagharibi nii haramu"-hii ni kwa lugha ya kihausa-lugha maarufu huko kaskazini mwa Nigeria na ndio nadharia kuu ya madhehebu hayo.Baadhi ya wafuasi wake walijiuzulu katika kazi zao za khubiri chuo kikuu walipojiunga na madhehebu hii.

Mchambuzi mmoja wa madhehebu hii anayaeleza hivi:

"Hoja zao zasema chanzo cha shida za kijamii tulizo nazo,umasikini,kuanguka kwa uadilifu kunatokana na wasomi walioelimishwa kimagharibi katika jamii yetu."

Yusuf Mohammed alieuwawa jana usiku, aliezaliwa 1970 ameacha wake 4 na watoto 12.Alikuwa tajiri mno na alipata elimu ya kimagharibi,lakini wafuasi wake waliotokana na makabila na hali tofauti kaskazini mwa Nigeria wanakoishi waislamu wengi,wanasema alielimishwa pia nchini Iran.

Waumini wa (Boko Haram) husali katika misikiti tofauti na ile ya waumini wengine katika miji kama v ile Maiduguri,Kano na Sokoto na wanaweka ndevu refu.Wanaamini wake zao wasionekane na wanaume wengine isipokuwa waume zao na mwiko lutumia vitu au zana za kimagharibi.Yeyote yuled asietii nadhariia yao iwapo ni mkristu au muislamu, anaangaliwa ni kafiri.

Rais Umaru Yar-Adua wa Nigeria, amesema vikosi vya ulinzi vimekuwa vikiichunguza madhehebu haya kwa miaka kadhaa na akayaeleza ni "Kitisho kikubwa" kwa usalama.Kwani, kikikusanya silaha na habari za upelelezi ili kuwalazimishja wanigeria kufuata nadharia yao.

Afrika magharibi kwa jumla, ina mila na desturi ndefu ya uislamu wa "SUFI ISLAM" usiofuata itikadi kali na unoshiikamana na udugu unajulikana kwa uvumilivu na hasa katika eneo la Sahel-kusiini mwa Jangwa la sahara upande wa pili mpakani na Nigeria.

Mwandishi:Ramadhan Ali/RTR

Mhariri:M.Abdul-Rahman