1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Misururu mirefu ya wanunuzi wa mafuta yashuhudiwa Nigeria

Grace Kabogo
31 Mei 2023

Mistari mirefu ilishuhudiwa jana nje ya vituo vya mafuta nchini Nigeria, siku moja baada ya rais mpya aliyeapishwa Bola Tinubu kutangaza kuondoa ruzuku ya mafuta.

https://p.dw.com/p/4S1dW
Msururu wa magari kama unavyoonekana katika picha iliyopigwa karibu na kituo cha mafuta cha Oando mjini Abuja, Februari 11, 2022.
Serikali mpya ya Nigeria hadi sasa haijatangaza hatua zozote za kuleta suluhisho kwa watumiaji mafuta. Picha: AFOLABI SOTUNDE/REUTERS

Matamshi hayo aliyatoa katika hotuba yake ya kwanza alipoapishwa siku ya Jumatatu. Hotuba ya Tinubu alizusha wasiwasi alipotangaza kuwa ruzuku ya mafuta imeondolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Petroli Nigeria, Mele Kyari, amesema ukweli ni kwamba serikali haiwezi tena kulipia ruzuku ya mafuta. Akizungumza jana na waandishi habari, Kyari amesea serikali inahitaji kulipa hadi naira trilioni 2.8 ambazo ni sawa na dola bilioni 6 kwa ajili ya ruzuku. Hata hivyo, amesema mazungumzo mengine yanaendelea ili kuleta unafuu kwa wananchi. Baadhi ya vituo vya mafuta ya petroli tayari jana vilianza kupandisha bei ya petroli, na hadi sasa serikali mpya haijatangaza hatua zozote za kuleta suluhisho kwa watumiaji mafuta.