1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mohammed Yusuf auawa akiwa mahabusi.

Abdu Said Mtullya31 Julai 2009

Kiongozi wa waislamu wenye itikadi kali ameuwa nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/J0bC
Watu waliokufa kufuatia ghasia nchini Nigeria.Picha: AP

ABUJA:
Maafisa  wa serikali nchini Nigeria wamesema   kiongozi wa waislamu wenye itikadi kali nchini humo  ameuawa kwa kupigwa  risasi. Kwa mujibu wa taarifa  rasmi kiongozi huyo Mohammed Yusuf aliuawa  wakati  akiwa mahabusi.

Mohammed Yusuf alilaumiwa  kwa mapigano yaliyonza jumapili iliyopita baina  ya wanajeshi wa  serikali  na wapiganaji wa kundi la waislamu wenye itikadi  kali nchini Nigeria,Boko  Haram.

Televisheni ya serikali ilionyesha mwili wake uliokuwa  umejaa matobo kutokana na  risasi.

Katika mapigano hayo watu  zaidi ya mia sita wameshakufa.

Waislamu  wenye itikadi kali wanapigania kupitishwa na kutumika sheria  za kiislamu nchini Nigeria kote.