1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigerian violence.

Abdu Said Mtullya29 Julai 2009

Rais Umaru Yar'Adua amesema atawazima waasi nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/IzFm
Nigeria yakumbwa na ghasia .

ABUJA.

Rais Umaru  Yar'Adua wa  Nigeria amesema  majeshi  ya  usalama yatawasaka  na  kuwazima  waasi waliobakia, wa kundi la waislamu waliosababisha mapigano  ambapo watu wasiopungua  150 waliuawa   katika siku tatu  zilizopita nchini Nigeria.


Ghasia zilizuka  mwishoni  mwa wiki iliyopita  baada ya  baadhi ya waumini wa kundi linalojiita  Boko Haram kukamatwa katika jimbo la Bauchi  kaskazini mwa Nigeria.

Kundi hilo linaloiga mfano wa taliban linapigania kupitishwa na kuenezwa  kwa sheria  za  kiislamu ambazo  tayari zinatumika katika miji 12 ya  kaskazini mwa Nigeria.

Mwaka jana watu 700 waliuawa katika mji wa  Jos, kutokana  na mapambano baina  ya  waislamu  na wakristo.