1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nimonia, kuhara magonjwa hatari kwa watoto

8 Juni 2012

Shirika linalohudumia Watoto la Umoja wa Mataia UNICEF limesema ugonjwa wa homa ya mapafu na kuharisha ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vya watoto wengi dunia hasa katika mataifa masikini.

https://p.dw.com/p/15Aw5
Watoto
WatotoPicha: AP

Kulinga na ripoti maalumu ya Umoja wa Mataifa ya Mfuko wa kuhudumia watoto inaonyesha kuwa magonjwa haya yanawauwa watoto milioni 2 kila mwaka sawa na asilimia 29 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano dunia nzima.

Taarifa ya Mkurungenzi wa UNICEF

Taarifa hiyo inaongeza kuwa mataifa yenye vifo vya watoto kwa wingi yanahitaji kuwapa tiba na jukumu kubwa ni utoaji wa chanjo na kuzishauri jamii zinazokumbwa na magonjwa haya kuhakikisha wanapata maji safi na salama, wanakuwa na njia bora za usafirishaji wa maji taka na kuwashauri akina mama kuwanyonyonyesha watoto hao maziwa ya mama.

Akizungumuzia hali hiyo Mkurugenzi msaidizi wa Shirika linalowahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Bi Geeta Rao Gupta amesema"Kwa mfano, maeneo masikini ya nchini nyingi hayapati maji safi wala hayana njia bora za usafirishaiji wa uchafu. Hali ya watoto katika mataifa masikini ni mbaya. Ukiangalia viashiria kadhaa, kwahiyo tunahitaji kulifanyia kazi hilo."

Watoto wakicheza pamoja
Watoto wakicheza pamojaPicha: UNICEF

Utoaji wa chanjo na changamoto

Hadi mwaka 2015 kutakuwa kumetokea vifo vya watoto milioni mbili kwa asilimia 75 ya mataifa ambayo yanakumbwa sana na homa ya mapafu na kuhara. Nusu ya vifo vya watoto duniani vinatokea katika mataifa matano ambayo ni: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria, Ethiopia, Pakistani na India. Japokuwa hali ni hiyo mataifa hayo yameendelea kutoa chanjo za Hemophilus Influenza B, Pneumococcal Conjugate na Rotavirus.

Kigingi kikubwa cha hali hiyo ni upatikanaji na usafirishaiji wa maji taka ambapo watu milioni 783 duniani hawapati maji safi ya kunywa na watu bilioni 2.5 duniani hawana njia bora za usafirishaji wa maji taka.

Asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na kuharisha vinatokana na uchafu na kukosekana kwa huduma bora za usafirishaji na utunzaji wa takataka katika mazingira wanayoishi binadamu.

Hali ya vifo vya watoto kwa magonjwa mbalimbali

Shirika hilo limesema asilimia18 ya vifo vya watoto ni kutokana na homa ya mapafu wakati asilimia 11 inatokana na kuhara.Wameshauri kuwa ni vyema mikono ikaoshwa kwa sabuni kabla ya kula na kutoka chooni.

Watoto wa Berlin wakicheza
Watoto wa Berlin wakichezaPicha: AP

Magonjwa mengine yaliyotajwa ni Ugonjwa wa UKIMWI unaosababisha vifo vya watoto kwa asilimia 2 na malaria kwa asilimia 7. Wakati hali ikiwa hivyo kwa ujumla mataifa ya bara Asia yanaonekana kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kutoka vifo milioni 2.2 mwaka1990 na kufikia vifo laki saba mwaka 2010.

Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE/DPAE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman