1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njama ya mapinduzi nchini Niger

Oumilkher Hamidou18 Februari 2010

KUndi la watu wasiojulikana wamefyetua risasi na kuripua mizinga mjini Niamey

https://p.dw.com/p/M4tC
Rais Mamadou Tandja wa NigerPicha: AP Photo

Risasi na mizinga inafyetuliwa mjini Niamey, mji mkuu wa Niger ambako duru zinazungumzia kuhusu njama ya kutaka kumpindua rais Mamadou Tandja.

"Kuna njama ya mapinduzi inayoendelea nchini Niger na rais Mamadou Tandja anajikuta katika hali dhaifu" amesema hayo afisa mmoja wa Ufaransa ambae hakutaka jina lake litajwe.

Kwa mujibu wa duru za idara ya upelelezi,na mashahidi,risasi zimeanza kusikika tangu mchana katika mji mkuu wa Niger- Niamey.Moshi unafuka toka kasri la rais.Haijuliakni lakini nani wako nyuma ya mashambulio hayo.

Afisa wa idara ya upelelezi ambae hakutaka jina lake litajwe amesema vikosi vya ulinzi wa rais vimeingilia kati kujaribu kuwatimua wanaandalizi wa njama hiyo ya mapinduzi.

Risasi zilihanikiza kwa karibu dakika 30 ,na baadae miripuko ikafuatia.Nyumba nzima imetikisika" amesema shahidi mmoja anaeishi mjini Niamey.Ameongeza kusema hata hivyo hali imeanza kuwa shuwari kidogo hivi sasa.

Kituo cha matangazo ya kimataifa cha Ufaransa-RFI kikiwanukuu mashahidi kimesema kwa upande wake milio ya risasi inaendelea kusikika hapa na pale.

Mshauri mmojawapo wa rais Mamadou Tandja amesema hata hivyo wanaidhibiti hali ya mambo.

Rais Mamadou Tandja aliyeingia madarakani tangu mwaka 1999 amelivunja bunge na kupitisha katiba iliyofanyiwa marekebisho Agosti mwaka jana kwa lengo la kuendelea kuwepo madarakani,baada ya mhula wake wa pili wa miaka mitano kumalizika december mwaka jana.Uamuzi huo umelaaniwa na jumuia ya kimataifa iliyotangaza vikwazo dhidi yake.

Licha ya mgogoro wa kisiasa uliofuatia kisa hicho na machafuko ya baadhi ya wakati ya watu wanaohama hama wa kabila la Touareg,makampuni makubwa makubwa mfano wa Areva la ufaransa au Cameco la Canada yamewekeza mabilioni ya dola nchini Niger nchi yenye kumiliki migodi mikubwa mikubwa ya maadini ya uranium.

Mwandishi:Oummilkheir Hamidou/AFP

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed